Saikolojia
Kwa Nini Watu Wengi Hawafanyi Wanachojua Wanapaswa Kufanya
Imeandikwa na Dr. Said Said · 2026-03-14 · 4 min read
(Na nini cha kufanya kuhusu hilo) Siku chache zilizopita, mmoja wa wanafunzi wetu alinitumia ujumbe. Ujumbe huo ulijaa maumivu na hali kuchanganyikiwa . Aliniam
(Na nini cha kufanya kuhusu hilo) Siku chache zilizopita, mmoja wa wanafunzi wetu alinitumia ujumbe. Ujumbe huo ulijaa maumivu na hali kuchanganyikiwa . Aliniambia kitu ambacho kimenigusa sana. Alisema: “Dr. Said, najua kabisa ninachotakiwa kufanya ili kufanikiwa. Najua natakiwa kupiga simu kwa leads, kufollow-up, kutengeneza content na kuuza. Lakini kila nikijaribu kufanya hivyo… najikuta sifanyi. Na ninajisikia vibaya sana. Naona kama ninapoteza kujiamini. Najiona kama mtu ambaye hawezi kujisimamia. Sina hata uhakika kwa nini hii inanipata.” Alisema anajisikia kama mtu aliyekwama , na anaanza hata kupoteza kujiamini kwake mwenyewe . Kilichoniumiza zaidi ni kwamba anajua kabisa nini cha kufanya . Lakini anashindwa kujisukuma kufanya. Kana kwamba amefungwa mnyoro mguuni asiweze kusonga mbele. Na mwisho wa ujumbe wake aliuliza: “Dr. Said, tatizo langu ni nini? Na nifanye nini?” Nilikaa nikafikiria sana kabla ya kumjibu. Lakini nilipokuwa nikifikiria, nikagundua kitu muhimu sana. Hili sio tatizo lake peke yake . Kwa uzoefu wangu, hili ni tatizo ambalo zaidi ya 70% ya wanafunzi wetu wanapitia . Watu wengi wanajua kabisa: nini wanapaswa kufanya hatua gani zinahitajika nini kitawapa matokeo Lakini bado wanashindwa kutekeleza hizo hatua kwa uthabiti . Hivyo nikaanza kuelezea jambo hili kwa kina. Tatizo Halisi: Sio Kukosa Maarifa Watu wengi wanafikiri kwamba tatizo lao ni kukosa maarifa . Lakini ukweli ni kwamba kwa watu wengi, maarifa tayari wanayo . Wanajua wanapaswa: kupiga simu kwa wateja watarajiwa kufanya follow-up kubandika matangazo kuandika content kuuza huduma zao Tatizo si kujua. Tatizo ni kutekeleza . Na mara nyingi tatizo la utekelezaji linatokana na vizuizi vya kisaikolojia . Tabaka za Kisaikolojia Zinazozuia Watu Kuchukua Hatua 1. Tabaka la Utambulisho (Identity) Hili ndilo tabaka la ndani kabisa. Watu wengi wanafanya mambo yanayolingana na identity yao ( imani yao kuhusu wao ni nani) . Kama mtu anaamini ndani yake kwamba: “Mimi si mtu wa nidhamu” “Mimi si muuzaji mzuri” “Mimi ni mtu mwenye haya” “Biashara sio kitu ninachokiweza sana” Basi vitendo kama: kupiga simu kwa wateja kuuza kwa ujasiri kujitangaza mtandaoni vinaonekana sio vya kawaida kwa yeye . Hivyo ubongo wake unaanza kuleta upinzani . Sio kwa sababu ni mvivu. Bali kwa sababu ubongo wake unajaribu kulinda utambulisho wake wa sasa . 2. Tabaka la Imani (Beliefs) Watu pia hutenda kulingana na imani walizonazo kuhusu jambo fulani . Mfano wa imani zinazoweza kuzuia hatua: “Kupiga simu haifany