Stratejia

Kwa Nini Baadhi ya Ofa Huwafanya Watu Watafute Pesa Haraka Ili Wanunue?

Imeandikwa na Dr. Said Said · 2026-04-05 · 8 min read

Hebu nikwambie ukweli ambao watu wengi hawausemi… Watu hawanunui kwa sababu umekuwa na bidhaa nzuri. Na hawanunui kwa sababu umetangaza bei ya ofa. Na mara nyin

Kwa Nini Baadhi ya Ofa Huwafanya Watu Watafute Pesa Haraka Ili Wanunue?

Hebu nikwambie ukweli ambao watu wengi hawausemi… Watu hawanunui kwa sababu umekuwa na bidhaa nzuri. Na hawanunui kwa sababu umetangaza bei ya ofa. Na mara nyingi hawanunui kwa sababu umeandika “ofa inaisha leo.” Wananunua pale wanapohisi kitu kimoja: “Nikikosa hii, nitaumia.” Hapo ndipo uchawi wa ofa kubwa ulipo. Na ukishalielewa hilo… Utaanza kuona kwa macho tofauti kabisa kwa nini baadhi ya watu mtandaoni huuza kwa nguvu sana… kwa nini wengine wanaandika tangazo moja na wanaingiza pesa nyingi… na kwa nini wengine wana bidhaa nzuri kabisa, lakini hawauzi karibu chochote. Tatizo si bidhaa peke yake. Tatizo ni ofa. Na mara nyingi, ofa dhaifu huua bidhaa nzuri. Lakini ofa kali… inaweza kubeba hata bidhaa ya kawaida na kuifanya ionekane ni nafasi ya kipekee. Sasa swali ni hili: Ofa zinazofanya watu wawe na hamu kali ya kununua zina sifa gani? Jibu ni hili… Ofa hizo huwa zinamfanya mnununuzi ahisi mambo manne kwa wakati mmoja: Anaitaka Anaiamini Anaiona ina thamani kubwa Anaona si busara kuchelewa Ukikosa moja ya hivi, mauzo hupungua. Ukivipata vyote vinne kwa pamoja… hapo ndipo unapata offer ambayo inawafanya watu waseme: “Sina pesa yote sasa hivi… lakini ngoja nitafute namna.” Na hapo ndipo mchezo wote unaanzia. 1. Offer Kubwa Huuza Matokeo, Sio Kitu Chenyewe Hili ndilo kosa kubwa ambalo watu wengi hawalioni. Watu wengi wanajaribu kuuza: kozi huduma bidhaa vifurushi consultation usajili Lakini mnununuzi hajali sana hayo. Mnununuzi anachojali ni hiki: “Hii itanifikisha wapi?” Hajali unanipa video ngapi. Hajali kama madarasa ni 12 au 25. Hajali kuna PDFs au ebook za bure. Anachojali hi hii: itanisaidia kupata nini? itanitoa kwenye tatizo gani? itanifikisha kupata matokeo gani? na kwa muda gani? Ndiyo maana offer kali haisemi: “Tunatoa mafunzo ya biashara.” Hiyo ni dhaifu. Offer kali husema: “Tutakusaidia kupata wateja wako wa kwanza.” au “Tutakusaidia kuongeza mauzo yako bila kubahatisha.” au “Tutakusaidia kufika hatua fulani ndani ya muda fulani.” Mnununuzi akiona matokeo kwa uwazi, akili yake inaanza kusogea. Kwa sababu sasa haoni “bidhaa” Anaona future yake . Na watu hununua future wanayoitamani. 2. Ofa Kali Humfanya Mnununuzi Aone: “Hii Ina Thamani Kubwa kuliko Pesa Ninayotoa” Hapa ndipo siri ya pili ilipo. Watu hawalalamikii bei kila mara kwa sababu bei ni kubwa. Mara nyingi wanalalamika kwa sababu hawajaona tha ya kutosha . Hii ni tofauti kubwa sana. Mtu anaweza kukataa kununua kitu cha shs. 100,000. Lakini akanunua kitu cha shs. 1,000,000 bila shida. K

Rudi kwenye Blog