Blog

Jinsi ya Kutimiza Malengo Mwaka 2026 Piga Ua

Imeandikwa na Dr. Said Said · 2025-12-03 · 10 min read

Kwanini Umekuwa Ukihangaika Kutimiza Malengo Yako Kila Mwaka Tabia hii inawamalize watu wengi mno… Baada ya sherehe na shamrashamra za mwaka mpya kupita, kijana

Jinsi ya Kutimiza Malengo Mwaka 2026 Piga Ua

Kwanini Umekuwa Ukihangaika Kutimiza Malengo Yako Kila Mwaka Tabia hii inawamalize watu wengi mno… Baada ya sherehe na shamrashamra za mwaka mpya kupita, kijana anajikuta yupo chumbani peke yake akitafakari na kujiuliza swala la msingi, “ Hivi nimefanya jambo gani la maana mwaka jana? ” Na bila ya kufikiria sana, jibu linamuangalia uso na macho. HAKUNA HATA KIMOJA CHA MAANA ULICHOKIFANYA! “ Kipato chako hakijaongezeka!” “ Kitambi chako hakijapotea!” “ Mahusiano yako na watu wa karibu yamezidi kuwa mabaya” Ukiulizwa vipi maisha? Bado unasema kuwa maisha magumu Ukiulizwa lini yatakuwa rahisi? Unasema “ One day Yes ” Lakini kinachokumaliza sio hayo majibu, bali vitu utakavyofanya baada ya kupata hayo majibu. Kwa vile upo Januari, unajitia moyo na kusema, “ Huu ndio mwaka wangu ” “ Mwaka huu mambo yatakuwa tofauti ” Mzuka unapanda, na pengine unaamua kukaa chini na kuandika ndoto zako kwenye “dream book” yako. Siku inayofuata unaanza kuyafanyia kazi. Unapambana kwenye biashara yako Unaamka mapema na kufanya mazoezi Unajaribu kuwa mtu bora kwa watu wanaokuzunguka “ Yes! Mwaka huu ndio mwaka wangu ” unajisemeza Wiki 2 zimepita lakini… Ukiangalia biashara yako haijakuwa! Ukiangalia kitambi chako hakijapungua Ukiangalia wanaokuzunguka, wanazidi kukuchukia “Mbona sioni mabadiliko?”Unajiuliza Hupati majibu. Na hapo ndipo unaishia kufanya jambo ambalo 91% ya watu hufanya Unakata tamaa! Mafanikio yamekuwa chungu. Huna hamu ya kufanya chochote. Unarudi katika maisha yako ya zamani ya kuhangaika na kufeli hadi January ijayo na kurudia kusema teana kwa mara nyengine… “ Huu ndio mwaka wangu ” “ Mwaka huu mambo yatakuwa tofauti ” Lakini mimi na wewe tunafahamu story yake itaishia wapi Je huyo ni wewe? Ushachoka kujiahidi kuwa mwaka huu utatoboa lakini unajikuta unavutwa pale pale ulipoanza? Kama jibu ndio, Usijali! Katika makala hii nitakupatia formula thabiti na tofauti. Formula ambayo sio tu itakufanya usikate tamaa, bali na kufanya mafinikio kuonekana rahisi kuliko kufeli. Jinsi ya Kutimiza Malengo Yako Mwaka Huu Piga Ua Chukulia mfano upo sehemu A unataka kuenda sehemu B, na kinachokuzuia kufika sehemu B ni kuta tatu zilizopo baina ya sehemu hizo mbili. Kama unataka kutimiza malengo yako PIGA UA basi huna budi isipokuwa kubomoa kuta hizo. Habari mbaya nikuwa kila kuta inayofuata ni ngumu zaidi kuibomoa kuliko iliyotangulia. Wengi wanafanikiwa kubomoa kuta ya kwanza lakini wanafeli katika kubomoa kuta mbili zinazofuata. Kuta hizo ni zipi na unazibomoaje? Kuta ya 1: BAYA

Rudi kwenye Blog